You Are Here: Home » Our Services » TANAPA YATAKIWA KUTOA ELIMU KWA UMMA

TANAPA YATAKIWA KUTOA ELIMU KWA UMMA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetakiwa kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutovamia maeneo ya Hifadhi za taifa kwa kuweka makazi na shughuli ufugaji na kilimo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana (MB) alipo kutana na uongozi huo katika ofisi zake zilizopo Hifadhi ya Taifa Mikumi Mkoani Morogoro.

Mhe Chana amesema si vyema kuona migogoro kati ya wanyama na watu walio vamia maeneo ya Hifadhi ikiendelea, hivyo ipo haja ya haraka ya kuielimisha jamii juu ya ukweli kuhusu namna bora ya kuepukana na migogoro hiyo hasa kwa wanaofanya kazi za kijamii kwenye mapito ya wanyama kama vile Tembo.

Licha ya kuzungumzia fursa zitakazo tokana na Filamu ya Royal Tour, Mhe Chana ameutaka uongozi wa Shirika hilo kuhakikisha linakaa na wananchi majirani na Hifadhi pamoja na wadau mbalimbali kuwaelimusha juu ya namna ya kuchangamkia fursa hiyo hasa katika kuwekeza katika Malazi, vyakula, na mazao mengine ya Utamaduni.

Akielezea changamoto wanazokutana nazo Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Steria Ndaga, ametaja kuwa ni pamoja na Utalii wa bure unaofanywa na wenye magari yanayopita   Hifadhini na kuisababishia Serikali kupoteza mapato makubwa, Moto, ukame nk

Akiwa Hifadhi ya Mikumi Mhe Chana alipa nafasi ya kutembelea vivutio vya Hifadhi hiyo na kujionea utajitri Mkubwa wa wanyama, mimea mbalimbali pamoja na ukarabati unaoendelea wa kiwanja cha Ndege.

© 2023 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top