You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AZINDUA MPANGOKAZI WA KUONGOA SHOROBA ZA WANYAMAPORI NCHINI

WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AZINDUA MPANGOKAZI WA KUONGOA SHOROBA ZA WANYAMAPORI NCHINI

WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AZINDUA MPANGOKAZI WA KUONGOA SHOROBA ZA WANYAMAPORI NCHINI

Wizara ya Maliasili na Utalii imezimdua, Mpangokazi wa kuongoa shoroba za wanyamapori nchini (Wildlife Corridors Assessment, Prioritization and Action Plan) ili kurejesha, kulinda na kuimarisha uhifadhi wa mapito ya asili ya wanyamapori na kukabiliana na changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Akizindua Mpangokazi huo jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema, kuwepo kwa shughuli za kibinadamu katika maeneo a mapito ya wanyamapori kunasababisha wanyamapori wasiweze kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa migongano baina ya wanyamapori na binadamu.

“Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo kwa kiwango kikubwa vinatokana na uwepo wa wanyamapori wa aina mbalimbali kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

“Matokeo haya chanya ni kutokana na uongozi mzuri wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao umeimarisha ulinzi katika maeneo yaliyohifadhiwa na kudumisha amani nchini”. Amesisitiza Waziri Balozi Dkt. Chana

Aidha Waziri Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa Wizara anayoingoza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi hususan USAID - Tuhifadhi Maliasili imefanya kazi kubwa ya tathmini ya shoroba zote za wanyamapori zilizopo nchini ili kuzitambua na kuandaa mpangokazi utakaosaidia kukabiliana na changamoto ya migongano ya wanyamapori wakali na waharibifu.

“Leo tunazindua Mpangokazi wa kuongoa shoroba za wanyamapori nchini. Nitoe rai kwa wadau wote wa uhifadhi kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuutekeleza mpango huo” Alisema Waziri Balozi Dkt Chana.

© 2023 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top