UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA TAASISI YA UTAFITI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWIRI)
Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumteua Dkt. David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 6(1)(2) cha Sheria ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Sura ya 260, kikisomwa pamoja na Jedwali la Pili, Kipengele Na. 1(1)(b)-(c), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI): -
1. Dkt. Maurus January Msuha, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii.
2. Bw. William Simon Mwakilema, Kamishna wa Uhifadhi, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
3. Bw. Needpeace Jonathan Wambuya, Naibu Kamishna, Huduma za Shirika, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
4. Bw. Mabula Misungwi Nyanda, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
5. Brigedia Jenerali (Mst), Mary Bayu Hiki.
6. Prof. Jafari Ramadhani Kideghesho, Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka.
7. Dkt. Amani Ngusaru, Mkurugenzi Mkazi, Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF)
8. Bi. Mercy Ezekiel Mrutu, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Aidha, Dkt. Eblate Ernest Mjingo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) anakuwa Katibu wa Bodi hiyo. Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 07 Novemba, 2022 hadi 06 Novemba, 2025.