You Are Here: Home » Whats New » TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU USWISI

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU USWISI

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU USWISI

Tanzania inashiriki Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaoendelea katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka na Mhe. Balozi Maimuna Tarishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva.
Miongoni mwa Ajenda ambazo Tanzania imejipanga kuzungumza ni pamoja na Haki ya Maendeleo kwenye Sekta ya Elimu, Afya, makazi, maji salama na Usafi.
Aidha, mkutano huo pia utaongelea athari za UVIKO 19 katika sekta ya Utalii na mikakati madhubuti iliyowekwa ya kudhibiti uchumi dhidi ya janga hilo ikiwemo kuhimiza utoaji wa chanjo ya uviko na kutangaza nchi kupitia Filamu ya Royal Tour ambayo imekuwa na matokeo chanya kutokana mwitikio mkubwa wa ujio wa watalii nchini Tanzania.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top