You Are Here: Home » Whats New » WIZARA YATENGA SH.700 MILI0NI KUWEZESHA UFUGAJI NYUKI KISASA

WIZARA YATENGA SH.700 MILI0NI KUWEZESHA UFUGAJI NYUKI KISASA

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) imetenga kiasi cha Sh700milioni kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufuga nyuki kwa njia ya kisasa kwa mikoa nane.

Kauli hiyo imetolewa leo Mbogwe katika mkoa wa Geita na Naibu Waziri wa Maliasili na Utaii, Mhe,Constanine Kanyasu wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Ametaja baadhi ya   wilaya katika mkoa wa Geita zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni wilaya ya Ushirombo pamoja na Mbogwe.

Kufuatia hali hiyo, Mhe. Kanyasu amezitaka wilaya hizo kujiepusha na ukataji miti ovyo kwa vile nyuki ni rafiki wa mazingira badala yake zijikite zaidi katika kupanda miti.

Akizungumzia kuhusu fungu hilo, Mhe, Kanyasu amewataka wakazi wa wilaya hizo wajiunge katika vikundi ikiwa ni moja ya vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji wa pesa hizo kwa ajili ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa.

Aidha,Naibu Waziri huyo amesema wafugaji hao wataokakuwa wamejiunga katika vikundi hivyo watapatiwa elimu ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa pamoja na kuwezeshwa pesa zitakazotumika kwa ajili ya kununulia mizinga ya kisasa itakayosaidia kuzalisha mazao ya nyuki yatakayokidhi soko la kimataifa,

Ameongeza kuwa baadhi ya pesa hizo zitatumika katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia wafugaji hao kuchakata na kufungasha mazao ya asali yenye viwango bora duniani.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa tayari Wizara imepata soko la uhakika la asali watakayoizalisha.

Ameongeza kuwa licha ya nchi ya Tanzania kusifika katika uzalishaji wa asali kwa wingi,,Wafugaji walio wengi wamekuwa wakifuga nyuki kimazoea

Kufuatia hali hiyo amesema Wizara imedhamiria kuleta mapinduzi katika uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuwawezesha wananchi kufuga kisasa hali itakayosaidia wananchi kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuhifadhi misitu.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top