You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO UTAKAPOJENGWA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA STIEGLER’S GORGE

WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO UTAKAPOJENGWA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA STIEGLER’S GORGE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji - Stiegler's Gorge kutasaidia kukuza utalii katika Pori la Akiba la Selous

Pia amesema mara baada ya kukamilika kwa mradi huo utasaidia sana katika kulinda na kuhifadhi mazingira,Hivyo kutakuwa hakuna mtu yeyote atakayekuwa akikata miti kwa ajili ya nishati ya kuni na mkaa kwa sababu kutakuwa na umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

Amefafanua kuwa kila mwananchi hata yule mwenye kipato cha chini atakuwa na uwezo wa kupika kwa kutumia nishati ya umeme hivyo matumizi ya mkaa na kuni yatapungua kwa kiasi kikubwa katika jamii.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo utakapojengwa mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge uliopo katika Pori la Akiba la Selous wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliongozana na baadhi ya Mawaziri akiwemo Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani, Waziri wa Kilimo, Mhe. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula pamoja Makatibu Wakuu na Watumishi mbalimbali.

Aidha, Amesema mradi huo utakapojengwa,  Pori la Akiba la Selous litakuwa likipokea watalii wengi kwa vile miundombinu kama vile barabara pamoja umeme vitakuwa vya uhakika

Amesema hadi sasa barabara tatu tofauti zimeshaanza kutengenezwa ambapo barabara mbili zitakuwa za kiwango cha changarawe na moja itatengenezwa kwa kiwango cha lami.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top