You Are Here: Home » Whats New » NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AUNGURUMA NCHINI KENYA, ATOA MSIMAMO WA TANZANIA

NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AUNGURUMA NCHINI KENYA, ATOA MSIMAMO WA TANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa msimamo kuwa Tanzania ipo tayari kuridhia mkataba wa mwaka 2001kwa nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu uhifadhi wa urithi wa utamaduni wa majini kama masharti iliyoyatoa yatatekelezwa.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo wa Kikanda wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni uliomo majini uliofanyika katika mji wa Malindi nchini Kenya, Mhe.Kanyasu amesema mkataba huo utahusu utafutaji wa malikale zilizomo majini zikijumuisha miji iliyozama “sunken cities” meli, ndege, vipande vya vyungu, sarafu   mashua pamoja na boti.

Akibainisha kuhusu msimamo huo,  Mhe.Kanyasu ameitaka UNESCO iwajengee uwezo wataalamu wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni uliomo majini ili waweze kubaini na kuweka kumbukumbu za maeneo yote yenye Malikale hizo  
                       

Pia , Mhe.Kanyasu amesema Tanzania inahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine zilizoridhia mkataba huo pamoja na kuimarisha mashirikiano kati ya nchi zilizoridhia na ambazo hazijaridhia ili kubadilishana uzoefu na utaaalam

Aidha, Ametaka mkataba huo uzingatie maslahi mapana ya nchi ili usizuie uvunaji wa rasilimali nyingine kwenye eneo ambalo lipo katika Mkataba.


Mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku mbili uliweza kuwakutanisha Mawaziri kutoka nchi za Tanzania,Comoro,Djibouti, Ethiopia,Madagascar,Shelisheli,Somalia Afrika Kusini na wenyeji Kenya pamoja na wajumbe kutoka Rwanda na Ertirea

Amesema endapo mkataba huo utaridhiwa utatekelezwa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na UNESCO pamoja na Ubalozi wa Uholanzi na tayari taratibu za utekelezaji wa mpango huo zilishaanza mwaka 2006.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top