You Are Here: Home » Whats New » MHE. KANYASU ATOA ANGALIZO PORI LA SWAGASWAGA. KUHUSU HOSTELI ZA WATALII

MHE. KANYASU ATOA ANGALIZO PORI LA SWAGASWAGA. KUHUSU HOSTELI ZA WATALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameuagiza Uongozi wa Pori la Swagaswaga kumsimamia Mkandarasi anayejenga Hosteli ya kulala watalii wapatao 77 kutokana na Mkandarasi huyo kuwa na rekodi isiyoridhisha ya kutokumaliza majengo ya serikali.


Pia, Ameutaka Uongozi huo kuwa makini na vifaa vya ujenzi anavyovitumia Mkandarasi huyo katika ujenzi wa jengo hilo utakaogharimu zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 250 baada ya kubainika kuwa baadhi ya tofali zinazotumika kuwa chini ya kiwango.

Hayo yameyasemwa na Naibu Waziri huyo wakati alipotembelea ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuhudumia watalii 77 kwa mara moja inayojengwa katika Pori hilo katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na kutaka hosteli hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa na kwa kiwango chenye ubora kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Kanyasu alifika katika jengo hilo na kujionea tofali zilizoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo zikiwa zimekatika vipande vipande.

 

Hali hiyo imempelekea Naibu Waziri Kanyasu kuagiza tofali hizo zikapimwe kwenye mamlaka husika kama zinakidhi viwango kwenye ujenzi wa jengo hilo.

 

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri Kanyasu ameuthadhalisha Uongozi huo kuwa makini na hatua za ujenzi wa jengo hilo la sivyo wataingia kwenye matatizo makubwa.

“Nawaagiza simamieni kwa kila hatua za ujenzi wa majengo hilo, mambo yakiharibika hamtakuwa salama ni lazima tuhakikishe thamani ya fedha inaendana na jengo halisi” alisisitiza Kanyasu.

Aidha, Ameutaka Uongozi huo uhakikishe vifaa vya ujenzi anavyovitumia Mkandarasi huyo ni vile ambavyo vimeandika kwenye mkataba na si vinginevyo.

Katika hatua nyingine Mhe. Kanyasu alitembelea jengo la ofisi za Pori hilo ambalo linaendelea kujenga katika eneo la Kwa mtoro na kuutaka Uongozi huo kusimamia kwa ukaribu majengo yote yanayoendelea kujengwa kwa ajili ya manufaa ya Pori hilo.

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top