You Are Here: Home » Whats New » HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN, YA KUZINDUA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI-NGORONGORO

HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN, YA KUZINDUA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI-NGORONGOROAwali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha sote kuwepo mahali hapa katika tukio hili la kihistoria. Aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika hafla hii ya uzinduzi wa Makumbusho mapya ya Olduvai.

Nina furaha kujumuika nanyi leo katika eneo hili la Bonde la Olduvai ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.  Hii ni mara yangu ya pili kutembelea eneo hili la Olduvai; mara yangu ya kwanza ilikuwa mwaka 2006 nikiwa Waziri wa Utalii wa Zanzibar na nilipata fursa ya kutembelea makumbusho ya zamani; hivyo nina furaha leo kuweza kujumuika nanyi katika uzinduzi wa makumbusho haya mapya na makubwa zaidi ambayo yamejengwa kisasa zaidi.

Wageni Waalikwa;
Makumbusho ni Taasisi muhimu katika kila Taifa duniani, mahali ambapo urithi wa utamaduni na wa asili wa nchi huoneshwa kwa faida ya watu wote.  Makumbusho hii ninayoifungua leo inaonesha mali kale ambazo ni kielelezo cha maisha na ustaarabu wa vizazi vilivyopita ambazo zinatusaidia sisi kujua tulipotoka na kujitambua vizuri.

Aidha, uzinduzi huu ninaoufanya leo unaendana na malengo tuliyojiwekea ya kuongeza na kukuza Vivutio vya Utalii ili kuvutia wageni (watalii) wengi zaidi kutembelea nchini kwetu.  Makumbusho haya yanazinduliwa hapa Olduvai/Ngorongoro kama tunavyojua mahala ambapo pana historia kubwa na ushahidi wa kisayansi wa mabadiliko ya Utu wa Mwanadau.

Jiografia ya Ngorongoro kwa ujumla imejipambanua kuwa ni eneo la kitalii lenye utajiri wa historia pana na urithi wa utamaduni, usanii na usanifu wa uasili uliowafanya wana historia duniani kukubaliana kwamba Ngorongoro ni eneo muhimu la kisayansi inayohusika na mabadiliko ya ubinadamu (Zamadamu na maendeleo yake.

Katika makumbusho hii tunashuhudia jinsi gani vizazi vilivyopita viliweza kumudu na kuishi katika mazingira ambayo yalikuwa yanabadilika badilika kila mara,  Kwa   mfano,  hapa   bonde la

Olduvai, zamadamu wa miaka milioni 2 iliyopita, waliweza kutengeneza zana za mawe kwa ajili ya kuchuna na kukatia nyama na kupasua mifupa.  Hii inaonesha kuwa, ulaji wa nyama ulikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo na mabadiliko ya mwanadamu tangu miaka milioni 2 hadi sasa.  Vile vile, zana hizi za mawe yamkini zilitumika kuchimbia mizizi ambayo ilikuwa chakula chao.  Kule Laetoli, nyao za zamadamu zinaonesha kuwa zamadamu walianza kusimama wima na kutembea kwa miguu miaka million 3.6 iliyopita.  Katika eneo la Engaruka takribani miaka 1,500 iliyopita Jamii ziliweza kuwa na mifumo mbalimbali ya umwagiliaji maji mashambani. Mifumo hiyo iliwawezesha kujihakikishia uwepo wa chakula cha kutosha na kuepukana na majanga ya njaa.  Malikale ndio chanzo cha utambulisho wa jamii popote pale duniani.

Malikale huwapatia watu falsafa ya kujitambua, kujua uhusiano wao na dunia, mazingira pamoja na mtazamo wao wa Dunia.

Kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya na mchango wa Serikali ya Tanzania, eneo la Bonde la Olduvai limepata sura mpya nzuri inayoendana na hadhi yake sasa. Aidha, maendeleo haya yameongeza na kuleta fursa nyingi za ajira kwa jamii ya kitanzania na kimataifa kupitia shughuli za uhifadhi na utalii wa eneno hili. Kama mgeni alikuwa apite tu sasa atatumia siku nzima kutazama na kufurahia eneno hili.  Natamani sana kuona kilichofanyika mahali hapa kikafanyike maeneno mengine yote yenye rasilimali hizi kama Nyayo za Zamadamu wa Laetoli hapa katika Hifadhi ya Ngorongoro, Mapango ya Amboni huko Tanga, Michoro ya Miambani ya Kondoa, Dodoma, Miji Mikongwe ya   Zanzibar,  Bagamoyo,  Kilwa   Kisiwani na   Songo   Mnara.

Nafahamu sana mahitaji makubwa ya utaalam na fedha zinazohitajika kutambua, kuhifadhi na kuendeleza maeneo hayo na mengine mengi ambayo bado hatujayafahamu. Maeneo haya ni ya muhimu sana katika kuhifadhi historia na utamaduni   lakini

pia yataongeza fursa zaidi za ajira kwa vijana wetu kupitia utalii wake.  Ni muhimu sana kwa wazawa wa maeneo haya wakafaidika na fursa hizi za ajira.

Hapo nitoe rai kwa Wataalam kuwa muendelee kuwa wabunifu na uchakarikaji wa kuandika mawazo na kuwaomba wadau na washirika wetu wa maendeleo mliopo hapa hususani mabalozi kutuunga mkono kwenye jitihada hizi kwani huu ni uridhi wa Dunia na sio Tanzania peke yake.  Niseme kuwa Serikali inayo nia ya dhati ya kuikuza Sekta hii Kiutalii, ikiwa ndiyo chachu kuelekea kwenye kati.

Waheshimiwa Wageni Waalikwa;
Kupata makumbusho bora na ya kisasa kama hii, ni wazi kuwa imehusisha wadau wengi sana ambao sio rahisi kuwatamka wote kwa majina yao.  Kwa mara nyingine nawashukuru sana Jumuyia ya Umoja wa Nchi za Ulaya waliotoa fedha   zilizotumika   katika

ujenzi wa Makumbusho hii pamoja na majengo mengine katika kituo hiki kama lile la jamii kufanyia biashara, jengo la wageni kupata chakula, ukarabati wa Kambi ya Leakey, ambayo nimetaarifiwa pia kuwa inaandaliwa kuwa Makumbusho pamoja

na kugharamia shughuli zote zitakazopelekea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kuungana na maeneno ya wilaya za Karatu na Monduli kuwa na hadhi ya UNESCO Global Geopark – yaani eneo linalotambuliwa kidunia kuwa na vivutio muhimu vya utalii wa kijiologia. (Thank you very much our Brothers from the EU, we greatly value your contribution in helping us preserve our past. Indeed we do not take this for granted and as Malcom X once said a ‘man without any history is like a tree without roots’; therefore I wish to once again reiterate our profound appreciation to you for this kind gesture that will ensure that our great-grandchildren will have a past to show and not just in pictures and narrations but with vivid examples . Asanteni sana

© 2018 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top