You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI WA MALIASILI, DK. HAMISI KIGWANGALLA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA, DODOMA

WAZIRI WA MALIASILI, DK. HAMISI KIGWANGALLA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA, DODOMA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Oktoba 21,2017 amewasili Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Mjini Dodoma na kufanya mkutano na watumishi pamoja na wakuu wa taasisi ya Wizara hiyo.

Awali akiwasili Wizarani hapo, Waziri Dk. Kigwangalla alipata kupokelewa na viongozi wakuu wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu Aloyce Nzuki pamoja na Naibu Waziri Japhet Hasunga (MB) na kisha kutembezwa kwenye ofisi mbalimbali za wizara hiyo.

Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo,  Waziri Dkt. Kigwangalla aliwataka watumishi wote kuzingatia miiko ya kazi kwa kila mmoja kusimama kwenye nafasi yake kama mtumishi aliyehaminiwa na Serikali.

“Kwa pamoja tushirikiane kuijenga Wizara hii kama dhamana tuliopewa na Mh. Rais wetu. Sisi tumekuja hapa kusimamia yale yote ya dhana na malengo kusogeza mbele gurudumu la wizara hii.

Tunahitaji sana uzoefu wenu, ufanisi wenu kwani mutaongeza spidi kwa kila mmoja wenu..aliyekuwa anakamata majangili 5, aongeze juhudi akamate 10 ama zaidi,

Aliyekuwa analeta watalii wachache aongeze bidii alete wengi zaidi na wengine hivyohivyo” Dkt. Kigwangalla alisema wakati akiteta na watumishi hao.

Pia aliwataka wataalam wote kuzingatia ufanisi wao wa kazi awe Daktari, Profesa ama mzoefu wa muda mrefu basi anahakika watamsaidia katika kuinua Wizara hiyo
.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali. Gaudence Milanzi amemwakikishia Waziri Dkt. Kigwangalla ushirikiano mkubwa katika kazi.

Aidha, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo wamepata kuwasilisha mada mbalimbali za idara zao na namna ya utekelezaji majukumu yao

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top