You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI KIGWANGALLA ATUA KWA KISHINDO HISPANIA, AUNGURUMA

WAZIRI KIGWANGALLA ATUA KWA KISHINDO HISPANIA, AUNGURUMA

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita Wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour)

 


Kongamano hilo limefanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi ya Biashara ya Madrid (IFEMA) IFEMA is the Trade Fair Institution of Madrid

Katika Kongamano hilo, Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

“Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii pamoja na viwanda” Alisema

Aidha, Waziri Kigwangalla alitumia nafasi hiyo kwa kuutangaza ukanda mpya wa kusini mwa Tanzania ambao umejaliwa kuwa na vivutio vya Utalii vya kipekee vinavyopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi pamoja Pori la Akiba Selous.

Katika hatua nyingine , Waziri Kigwangalla wakati akizizima katika kongamano hilo aliwaeleza washiriki hao kuhusu juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Mhe.John Pombe Magufuli kwa kutaja mifano michache kama vile kufufua kampuni ya ndege (ATCL) kwa kununua ndege mpya sita pamoja kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha umeme katika mto Rufiji.

Aidha, Aliweza kutaja ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara.

Alibainisha kuwa kutokana na juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali hiyo, sekta ya utalii itaweza kusonga mbele ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri kwa watalii pamoja na wawekezaji kwa ujumla.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top