You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF

WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa mradi wa viwanda vya kusindika kuchakata na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda

Ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa akizindua Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo hata kama haitatekeleza mambo mengine yote ila suala la uanzishwaji wa viwanda ilitekeleze kwani suala hilo lina umuhimu mkubwa sana kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..
Ameongeza kuwa endapo suala la uanzishwaji viwanda lifanikiwa litaweza kuchochea jamii kuwa mstari wa mbele kulinda misitu badala ya sasajamii kujikita katika ukataji miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa jangwa kama hatua za haraka hazitachuliwa. 
Amesema kwa kiwango cha ufugaji nyuki kwa mikoa inayofuga   si cha kuridhisha kwa vile wafugaji walio wengi wamekuwa wakifuga kwa mazoe jambo ambalo wafugaji wengine wameamua kuachana na shughuli hiyo na kugeukia uchomaji mkaa pamoja na shughuli nyingine zinazoathiri mazingira
Waziri Kigwangalla amesema uanzishwaji wa viwanda hivyo vitasaidia jamii kuwa na kipato mbadala hali itakayopelekea wananchi kuanza kuona umuhimu wa kulinda misitu.
“Mkianza kuwekeza upande magharibi ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini wananchi, wakiwemo Nzega, Sikonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua hawatakubali kuona mtu au kikundi cha watu kinaharibu misitu.

“Nataka kuona mapinduzi makubwa kwenye ufugaji wa nyuki kwa kuiwesha jamii kuwa na mizinga ya kisasa ili iweze kufuga nyuki kisasa na hatimaye wapeleke kwenye viwanda, ifungashwe kisasa, ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.


Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa uhuishaji wa misitu ya kijiji pamoja na ile ya Halmashuri ambayo tayari imeharibiwa kwa kunza kupanda mitiya asili pamoja na kuanzisha mashamba mapya ya miti.

Awali, Kaimu Katibu ,Mkuu wa Wizara hiyo, Lusius Mwenda amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo umekuwa ukisaidia sana kwenye uhifadhi licha ya kuwa mfuko huo umekuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Ishengoma amemhakishia Waziri kuwa Wajumbe wa Bodi watafanya kazi kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu kuanza na suala la uanzishwaji wa viwanda vitavyowasaidia wafugaji nyuki nchini.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top