You Are Here: Home » Whats New » WATUMISHI WA MALIASILI WASHIRIKI KUMPONGEZA MHE.RAIS KWA SUALA LA KIKOKOTOO

WATUMISHI WA MALIASILI WASHIRIKI KUMPONGEZA MHE.RAIS KWA SUALA LA KIKOKOTOO

afanyakazi wa Maliasili na Utalii wameungana na Watumishi wa Umma wa Wizara na Taasisi za Serikali mbalimbali kushiriki maandamano yaliyoratibiwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha uzalendo wa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo cha Pensheni kwa Watumishi wa Umma waliostaafu.

Maandamano hayo yamefanyika leo Jumatatu Januari 7, 2019 kuanzia viwanja vya Bunge hadi viwanja vya Nyerere Square ambapo yamepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri w
a Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa Majaliwa.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top