You Are Here: Home » Whats New » UUZAJI WA MITI YA MISAJI (TEAK) KWA NJIA YA MNADA KATIKA MASHAMBA YA MITI MTIBWA (MOROGORO) NA LONG

UUZAJI WA MITI YA MISAJI (TEAK) KWA NJIA YA MNADA KATIKA MASHAMBA YA MITI MTIBWA (MOROGORO) NA LONG

1. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 8,067 zilizopo katika shamba la miti Mtibwa Mkoani Morogoro na Longuza Mkoani Tanga. Jumla ya meta za ujazo 3,170 na 4,897 zinatarajiwa kuuzwa katika shamba la miti Mtibwa na Longuza mtawalia. Mauzo haya yatafanyika Agosti 16, 2017 katika ofisi za shamba la miti Mtibwa saa nne na nusu (4:30) asubuhi na Agosti 18, 2017 katika ofisi za shamba la miti Longuza saa nne na nusu (4:30) asubuhi. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya Mnada (Auction) kwa kuzingatia kanuni 31 (ii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Miti hii ya Misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

2. Kampuni au mtu binafsi anayetaka kushiriki mauzo kwa njia ya mnada anatakiwa kuwasilisha maombi kwenye bahasha iliyofungwa kuonesha nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiambatisha, Usajili wa kiwanda cha kupasua magogo (Mwaka 2017/18) na cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN). Aidha, anatakiwa aoneshe namba ya kitalu/vitalu, bei na ujazo anaotarajia kununua kama ilivyo kwenye jedwali namba 1 na 2 hapo chini.


3. Mnada utaendeshwa hadharani wakiwepo wanunuzi wote katika ofisi za Mameneja wa mashamba siku ya Jumatano Tarehe 16 Agosti, 2017 kwa shamba la Mtibwa na Ijumaa Tarehe 18 Agosti, 2017 kwa shamba la miti Longuza. Mnada utaendeshwa kwa kufuata Sheria ya Misitu Sura 323.


4. Kila kiunga kitanadiwa peke yake kulingana na bei ya ujazo iliyopo. Hata hivyo, bei ya juu iliyotolewa na mnunuzi wakati wa kufungua bahasha haitazuia wanunuzi wengine kuongeza bei zaidi ya iliyotajwa awali.

5. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unawaalika wanunuzi kutuma maombi yao kwa ajili ya kufanya  mnada katika Mashamba ya miti Mtibwa na Longuza ambapo mnunuzi anaweza kuchagua mojawapo kati ya vitalu vifuatavyo;


JEDWALI Na. 1: KIUNGA NAMBA MT 11 SHAMBA LA MITI MTIBWA
No Jina la Kitalu Ujazo kwa kitalu  (m3) Bei ya awali/kitalu/m3
1 MT 11- A1 264.3182 600,000
2 MT 11- A2 204.4551 600,000
3 MT 11- A3 200.1980 600,000
4 MT 11- A4 228.4520 600,000
5 MT 11- A5 280.1400 600,000
6 MT 11-H1 245.4266 600,000
7 MT 11-H2 191.5186 600,000
8 MT 11-H3 207.6209 600,000
9 MT 11-H4 172.3329 600,000
10 MT 11-B1 272.0060 600,000
11 MT 11-B2 242.8832 600,000
12 MT 11-B3 222.7314 600,000
13 MT 11-B4 208.5882 600,000
14 MT 11-B5 228.8615 600,000
JUMLA YA UJAZO 3,169.5326 

JEDWALI Na. 2: KIUNGA NAMBA KH2C SHAMBA LA MITI LONGUZA

S/N COMPATMENT NAME COMPATMENT VOLUME (m3) FLOOR PRICE PER COMPATMENT/m3
1 KH 2C-01 619.251 800,000
2 KH 2C-02 702.830 800,000
3 KH 2C-05 241.440 800,000
4 KH 2C-A1 428.332 800,000
5 KH 2C-A2 441.268 800,000
6 KH 2C-A3 426.542 800,000
7 KH 2C-A4 466.969 800,000
8 KH 2C-A5 424.853 800,000
9 KH 2C-A6 418.360 800,000
10 KH 2C-A7 393.096 800,000
11 KH 2C-A8 334.360 800,000
JUMLA YA UJAZO          4,897.301 

 

Angalizo:  Kila kiunga kitauzwa peke yake

6. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania utatoa hati ya ushindi kwa mnunuzi aliyetaja kiwango cha juu kwa kila kiunga wakati wa mnada.
7. Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa kusafiirisha magogo nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni ya 50(1) ya mwaka 2004. Kusafirisha Mazao ya Misitu nje ya nchi ni baada ya kuyachakata kwa Mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 69 la mwaka 2006
8. Watu binafsi na makampuni wanakaribishwa kutembelea viunga shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri isipokuwa siku za sikukuu. Meneja wa shamba au msaidizi atakuwepo kwa ajili ya maelekezo zaidi.
9. Wanunuzi wanapaswa kuchukua na kusoma masharti ya uvunaji kwa kila shamba yatakayopatikana kwa Meneja wa shamba husika.
10. Bei ya kianzio kwa kila plot (kiunga) imeoneshwa katika Jedwali namba 1 na 2 hapo juu ikijumuisha ‘VAT’, ‘CESS’ , ‘LMDA’ , TaFF na FOREST ROYALITY.
11. Mnunuzi atakayeshinda atalipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote ya ununuzi siku tatu (3) baada ya mnada kufanyika. Fedha hizo hazitarudishwa. Asilimia sabini na tano (75%) iliyobaki italipwa ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya mnada. Malipo yote yafanyike kwa kupitia mfumo wa makusanyo ya Serikali (GePG) baada ya kupewa Bill ya mfumo kupitia Bank ya NMB au M pesa. Bili inayoonesha kiasi cha kulipa itatolewa na Meneja wa shamba husika.
12. Mnunuzi atapaswa kuwasilisha hati ya malipo kwa meneja wa shamba husika kama uthibitisho wa malipo si zaidi ya siku tatu (3) baada ya malipo kufanyika.
13. Wanunuzi watakaoshinda watasaini mkataba na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania siku kumi na nne (14) baada ya kulipa salio la aslilimia sabini na tano (75%) ya gharama zote.
14. Tangazo la mnada huu linapatikana katika tovoti zifuatazo: www.tfs.go.tz, na www.mnrt.go.tz
15. Maombi yote yawasilishwe siku ya mauzo kabla ya saa 4:00 asubuhi. wanunuzi watakaochelewa kuwasilisha maombi yao kwa siku na muda uliopangwa hawataruhusiwa kushiriki katika mnada.

Iimetolewa na
MTENDAJI MKUU
S. L. P 40832

© 2018 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top