You Are Here: Home » Whats New » TANAPA YATENGA   3.9 BILIONI KUENDELEZA MAPORI YA AKIBA YALIYOPANDISHWA HADHI

TANAPA YATENGA   3.9 BILIONI KUENDELEZA MAPORI YA AKIBA YALIYOPANDISHWA HADHI

Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati akihitimisha bajeti ya Wizara mnamo Mei 22 mwaka huu mjini Dodoma alipotangaza Mapori ya Akiba matano kuyapandisha hadhi kutoka
Mapori ya Akiba na kuwa Hifadhi za Taifa, Mapori hayo ni Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika.

Hayo yalielezwa na Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, Damian Saru mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga alipotembelea jana mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) katika ziara yake ya siku tatu ya kikazi mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.

Mhifadi Mkuu huyo alitaja baadhi ya malengo la fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi, kuainisha mipaka kwa kuwashirikisha wananchi,  kujenga miundombinu ya utalii na utawala, kuweka mifumo ya kielektoniki ya ukusanyaji kodi, kuandaa na kuendeleza ,miundombinu ya utalii pamoja kuandaa na kuendeleza vivutio vya utalii.

Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi Hhizo, Saru alitaja baadhi ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo hadi hivi sasa alisema tayari askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Alieleza kuwa, Mashine ya kutengeneza barabara ’ Motor Grader moja imeshaletwa kwa ajili ya kutengenezea barabara.

Pia, Alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari manne, mahema silaha, GPS vimeshaletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi

Kufuatia utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio yaliyopatikana katika kopindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika kipindi cha wiki mbili ni pamoja na ng’ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Pia , Alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa ujangili wamekatwa pamoja na vifaa vilivyokatwa kama vile mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli zopatazo 10.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Hasunga ameipongeza TANAPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kwa nzuri wanazozifanya katika kipindi hiki cha mpito.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mhe. Hasunga amewaagiza TANAPA wahakikishe waboreshe barabara kwa haraka ili ziweze kupitika mwaka mzimu kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Aidha , Naibu Waziri Hasunga ametaka Wawekezaji wajitokeze ili waweze kuwekeza kwenye huduma za malazi pamoja huduma za utoaji chakula.


Mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi yalianzishwa rasmi mwaka 1963 na yanapatikana katika wilaya sita katika mikoa ya Kagera na Geita.

Kwa upande wa Mapori ya Akiba ya Ibanda na Rumanyika yalianzishwa rasmi mwaka 1974 yanapatikama katika wilaya ya Kyerwa na inapakana na vijiji 40.

 

 

 

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top