You Are Here: Home » Whats New » SERIKALI YAAGIZWA KUTAIFISHA MIFUGO ITAKAYOKUTWA KWENYE HIFADHI

SERIKALI YAAGIZWA KUTAIFISHA MIFUGO ITAKAYOKUTWA KWENYE HIFADHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewatahadhalisha wafugaji ambao ng'ombe zao ziliondolewa katika Mapori matano ya Akiba yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa na baadala yake wafugaji hao hao wameamua kuingiza ng'ombe hao katika misitu ya Hifadhi ya mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza.

Pia, Ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) iimarishe ulinzi katika misitu hiyo ili kudhibiti makundi ya ngombe ambayo yameonekana yakiingia katika Misitu hiyo na ng’ombe watakaowakamatwa ndani ya Hifadhi hizo wataifishwe mara moja kwa kufuata sheria.

“Nawaagiza TFS hakikisheni mnasimamia sheria, ng’ombe mtakaowakamata wakiwa katika maeneo yenu muwataifishe bila kuchelewa ila fuateni tu sheria. alisema Waziri Hasunga.


Maagizo hayo yametolewa mkoani Kagera alipokuwa akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Biharamulo katika ziara yake ya kikazi katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika.

Amewataka wafugaji hao waanze kuondoka mara moja na makundi hayo ya ng’ombe kabla hawajakamatwa kwa vile Wizara yake haiwezi kukubali misitu iharibiwe ilihali yeye yupo kwa ajili ya kazi hiyo.

Aidha, amewataka wafugaji hao watambue kuwa sheria inakataza kufanya malisho katika maeneo yaliyohifadhiwa, Hivyo wale wataokamatwa sheria itafuata mkondo wake.

Awali Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde wakati akisoma taarifa yake,  amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baada ya operesheni iliyokuwa ikifanyika mara kwa mara kwa ushirikiano na Jeshi la polisi pamoja na Kikosi Dhidi ya Ujangili(KDU) kanda ya Kaskazini Magharibi ya kuondoa mifugo, Kwa sasa Wafugaji hao wameamua kuanza kuingiza mifugo yao katika misitu ya Hifadhi..

Ameongeza kuwa kama jitihada za haraka hazitafanyika za kuwaondoa wafugaji hao, watachangia kuharibu misitu hiyo kama walivyofanya katika Mapori hayo matano hali iliyopelekea wanyamapori kuhama.

Aidha, Amemweleza kuwa makundi ya n’gombe hao wamekuwa wakionekana katika nyakati tofauti yakiingia katika Hifadhi hizo hali itakayosababisha uhalibifu wa misitu hiyo.


Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya TAWA , TANAPA pamoja na Ofisi yake vimechangia wafugaji kukosa pa kulishia mifugo yao hivyo wameamua kuvamia Hifadhi za Misitu.

Amemweleza kuwa TANAPA imeleta askari 58 mbali na wale askari wa TAWA, Hivyo wafuga wale wale waliondolewa katika mapori matano ya akiba wameamua kukimbilia upande wa pili baada ya huku kuona kila wakiingia kulisha mifugo yao wanakamatwa.

“Nakuomba tufanye ushirikiano na TFS pamoja na Kamati za ulinzi za mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza . tuanze kuwaondoa kama tulivyowaondoa katika Mapori hayo.

 

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top