You Are Here: Home » Whats New » RAIS MSTAAFU MWINYI AIFAGILIA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA SABASABA

RAIS MSTAAFU MWINYI AIFAGILIA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA SABASABA

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa juhudi inazozifanya za kuelimisha jamii kuhusu uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Uendekezaji Utalii.

Ametoa pongezi hizo leo wakati alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere.

Amesema ameridhishwa na namna waoneshaji walivyojipanga na jinsi walivyo mahiri katika kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu uhifadhi.

Aidha, Rais Mwinyi ametoa wito kwa jamii kuungana na serikali kulinda na kuhifadhi Maliasili zilizopo nchini kwa ajili ya maendeleo.

Akizungumzia kuhusu bustani ya wanyamapori hai, Rais Mwinyi amesema amevutiwa sana na wanyama pamoja aina mbalimbali ya ndege waliopo.

Pia, Rais Mwinyi ameitaka jamii kuendelea kulinda na kuhifadhi misitu kwa vile bila misitu hakuna wanyamapori.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu amemshukuru Rais Mwinyi kwa kutenga muda wake na kuchagua Banda la Wizara kuwa ni miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea.

 

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top