You Are Here: Home » Whats New » NAIBU WAZIRI KANYASU ASITA UGAWAJI MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

NAIBU WAZIRI KANYASU ASITA UGAWAJI MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameahidi kulifanyia kazi suala kugawa miche ya miti kwa Wananchi bure ili wakaipande iliyooteshwa na Kurugenzi ya Mbegu za miti kuwa utaratibu huo hauwezi kuleta matokeo yanayokusudiwa na Serikali.

Imeelezwa kuwa uzoefu uliopo unaonesha kuwa vitu vingi ambavyo Serikali imekuwa ikivigawa bure kwa Wananchi bila wananchi hao kuchangia gharama yoyote vitu hivyo hushindwa kuvithamaini.

Mhe. Kanyasu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 29, 2019 mkoani Morogoro wakati alipotembelea ofisi za Kurugenzi hiyo kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha Mbegu za miti ikiwemo ya mbao pamoja na matunda ambayo itasambazwa nchi nzima.


Amesema utaratibu huo itabidi uangaliwe upya kwa vile ni ngumu kwa wananchi walio wengi kuitunza kwa sababu hawasikii uchungu na walio wengi hujikuta wakiitupa au kuiacha bila kuimwagilia hadi inakufa.

Akitolea mfano chandarua zilizokuwa zimetolwa bure na serikali, Amesema wananchi walio wengi walijikuta wakizitumia kwenye shughuliz za uvuvi pamoja na kutengenezea uzio kwa ajili ya kuku.

‘‘Ukichukua miche halafu uipeleke mkoani Shinyanga ukagawe bure yote italiwa na ngombe na vivyo hivyo ukipeleka Dodoma ukagawe bure yote itakufa kwa vile haitamwagiliwa kwa sababu ni ya bure’’ Amesisitiza.

Amesema endapo mtu ataweza kuchangia pesa kidogo ya hiyo miche ya basi ataitunza kwa vile atakuwa na uchungu nayo huku akitegemea kuwa kuna siku atavuna matunda au atapata mbao.

Ameongeza kuwa utaratibu huo hauna tija kwa vile siku zote kitu cha bure hakithaminiwi, hivyo lazima kila Mwananchi achangie hata kiasi kidogo cha pesa lakini sio bure kabisa hiyo itamfanya aithamini.

Amesema miche ya miti ya inaweza kutolewa bure kwa taasisi ya umma kama vile shule kwa makubaliano maalumu ila sio kwa wananchi.

Aidha, Naibu Waziri Kanyasu ameitaka Kurugenzi hiyo ijiendeshe kibiashara badala ya kujikita tu kutoa huduma kwa wananchi,

‘‘Tunataka mzalishe mbegu bora,  lakini tunataka tuone mnazalisha kibiashara tofauti na ilivyo sasa’’ Amesema

Katika hatua nyingine, Mhe Kanyasu ameiagiza Kurugenzi hiyo ifungue utalii wa bustani wa miti na maua katika jiji la Dodoma ambao ni moja ya aina ya utalii ambao umeanza kupendwa na watu wengi duniani.

Amesema miji kama Arusha pamoja na Mwanza imeanzisha utalii huo licha ya kuwa umekoseka mwongozo maalum bapo kila mtu amekuwa akifanya ili mradi tu licha ya kuwa watalii wengi wa ndani nje ya nchi hasa wapenda mazingira wamekuwa wakimiminika katika bustani hizo.

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top