You Are Here: Home » Whats New » Maonyesho ya Utalii - Karibu Travel Market yafana Jijini Arusha.

Maonyesho ya Utalii - Karibu Travel Market yafana Jijini Arusha.

Maonyesho ya Utalii - Karibu Travel Market yafana Jijini Arusha.

Wizara ya Maliasili na Utalii imeungana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii jijini Arusha katika maonyesho ya 15 ya utalii maarufu kama Karibu Travel Market (KTM). Maonyesho haya ya siku tatu 6-8 Juni yanalenga kukuza fursa za utalii zilizopo nchini pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vilevile yanatoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu katika shughuli za utalii. Kwa mwaka huu nchi za Afrika Mashariki zilizoshiriki ni Uganda, Kenya na Rwanda. Washiriki kutoka Zimbabwe pia walijumuika kwenye maonyesho haya.

Maonyesho ya KTM yanatambua kuwa uhifadhi wa wanyamapori ndio msingi wa utalii, hivyo maonyesho ya mwaka huu kupitia Umoja wa waendesha utalii Tanzania (Tanzania Association of Tour Operators) wameonyesha jitihada zao katika kuendeleza uhifadhi endelevu nchini.

KTM imeleta pamoja wadau wote wa utalii wanaofanya shughuli zao moja kwa moja na wale ambao wanachangia shughuli za utalii kuboreshwa. Wadau hawa ni pamoja na kampuni za utalii, hoteli na migahawa, kampuni za simu, kampuni za magari, mashirika ya ndege, kampuni za usalama, taasisi za fedha n.k.

© 2018 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top