You Are Here: Home » Whats New » MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AFUNGUA MAONESHO YA UTALII YA KIMATAIFA (S!TE)

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AFUNGUA MAONESHO YA UTALII YA KIMATAIFA (S!TE)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mama Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mapato yatokanayo na utalii yanatarajia kukua hadi kufikia Dola za kimarekani USD 16 Bilioni ifikapo 2025.

Makamu wa Rais amesema hayo leo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua MaoneshoyaKimataifa ya Utalii (SITE), yaliyoanza leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

“Tuna mategemeo ya kufikia kiwango hicho cha pesa hivyo serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kuinua uchumi kupitia sekta ya utalii kwa kuweka mazingira mazuri kwa kuwa na Miundombinu ya kutosha ikiwemo barabara ,Mashirika ya ndege, Njia za maji pamoja na Mazingira mazuri ya biashara yautalii nchini hili kurahisishia sekta hii na wadau kufanya kazi kwa ufanisi ” amesama Makamu wa Rais Mama Samia.

Amesema kuwa serikali imejidhatiti katika kuinua sekta ya utalii nchini hivyo maonesho haya yataileta sekta hii nchini na wadau wengine kwa kuona fursa zilizopo na kushughulikanazo .

Makamu wa Rais amesema kuwa Tanzania imezidi kuwa sehemu bora Zaidi ya utalii Duniani kutokana na machapisho na tovuti nyingi kuelezavivutio vilivyopo.

Ametaja kuwa SafariBookings.com imetaja Tanzania ndio sehemu bora Afrika ya kufanyautaliikwakueleza alma kamaMlimaKilimanjaro ,Ngorongoro Crater na hifadhi ya Taifa ya Serengeti kama moja ya maajabu saba ya Dunia.

Aidha amesema kuwa Jarida la New York Times nalo limeitaja Tanzania kuwani sehemu bora katika ulimwengu kwaajili ya utalii pia mtandao wa Fox News.Com Umeleza kuwa Ngorongoro Kreta kuwa ni moja ya Sehemu nzuri ya kutembelea.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala amesema kuwa Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi ambavyo bado havijatangazwa kikamilifu kupitia fursa hiyo ya Maonesho watalii wengi wataweza kuvifahamu na kuvitembelea

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top