You Are Here: Home » Whats New » Makamu wa Rais, Dkt. Bilal Afungua Maonesho ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal Afungua Maonesho ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal Afungua  Maonesho ya Kimataifa ya  Swahili International Tourism Expo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amesema kuwa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii yajulikanayo kama ‘’Swahili International Tourism Expo (S!TE)’’ yamekuwa na mchango mkubwa sana katika kutangaza fursa zinazopatikana nchini hasa vivutio vya Utalii vya Kitanzania katika nyanja za Kimataifa

.Akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho hayo jana yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Mlimani City jijini Dares Salaam,  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amesema Utalii ni sekta yenye ushindani mkubwa hivyo kupitia Maonesho hayo washiriki watumie muda wa maonesho hayo kujifunza masuala mbalimbali ikiwa na pamoja na kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kuendesha biashara ya Utalii kwa ufanisi uliokusudiwa.

Amesemakwamba Maonesho ya ‘’Swahili International Tourism Expo ( S!TE)’’ ambayo yanafanyika kwa mara ya pili sasa hapa nchini yamekuwa na mwitikio chanya kwa washiriki kutoka pembe zote za dunia kutokana na umuhimu wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya Utalii kitaifa na kimataifa.

Amesema kwa mwaka jana jumla ya Washiriki walioshiriki ilikuwa ni 40 lakini kwa mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka hadi kufikia 110 ‘’’  Hongereni Bodi ya Taifa ya Utalii kwa kazi nzuri mliyoifanya katika kuwavutia washiriki wengi zaidi kukubali kushiriki’’ Dkt. Bilal alisema

Dkt. Bilal amesema Sekta ya Utalii imekuwa inakua kwa kasi sana hapa nchini kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Mhe. Rais Kikwete,  katika kujitangaza.
Hivi karibuni katika jitihada za kuhakikisha kuwa Utalii unakua, Mhe. Rais Kikwete alizindua tangazo maalum la Utalii liitwalo ‘’ Tanzania is a Soul of Africa’’ litakalorushwa kwenye vyombo vya habari vya Kimataifa kwa lengo la kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mahmoud Mgimwa   amesema kwamba Maonesho hayo yamekuwa na mvuto kutokana na makampuni ya ndege pamoja na makampuni ya usafirishaji ya watalii yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na Watalii kutoka Mataifa ya nje wamekuwa wakija nchini kwa ajili ya kuona vivutio tulivyo navyo kutokana na kuwa usafiri wa uhakika.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru, amesema   Maonesho ya ‘’Swahili International Tourism Expo (S!TE)’’ yaliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB)  yamekuwa muhimu sana kwa kuwa yamekuwa yakitangaza fursa zilizopo kwa wageni wa wenyeji ili waweze kuzichangamkia kupitia sekta ya Utalii.

Dkt. Meru, amesema kuwa Maonesho haya yatakuwa yakifanyika kila mwaka kwa lengo la kutangaza Utalii na kuyafanya maonesho haya kuwa ya Kimataifa na sio Afrika tu bali yawe ni ya kidunia.‘’Hii itasaidia sana kujifunza toka kwa wenzetu jinsi wanavyofanya Biashara za utalii’’ Dkt.Meru alisisitiza.

Pia,  Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii , Bi. Devota Mdachi amesema kwamba kupitia Maonesho hayo Tanzania itazidi kupata watalii wengi zaidi kutokana na mwitikio wa mataifa makubwa kukubali kushiriki katika maonesho hayo.


                                               

 

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top