You Are Here: Home » Whats New » Majina ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na chuo cha misitu Olmotonyi

Majina ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na chuo cha misitu Olmotonyi

Mkuu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha anayo furaha kuwataarifu wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha kwa udhamini wa binafsi, Wakala wa Huduma za Misitu na Mradi wa ECOPRC kwa mafunzo ya Astashahada na Stashahda za Misitu kwa mwaka wa masomo 2014/2015. TAFADHALI ZINGATIA: kwa wote waliochaguliwa kwa ufadhili binafsi ili kuthibitisha udahili na nafasi yako unatakiwa kulipa shilingi 200,000/- ikiwa ni sehemu ya ada ifikapo tarehe 11 Julai 2014. Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea kupoteza nafasi hiyo. Jina la mwekaji wa fedha katika fomu ya kuweka fedha benki liwe ni jina la mwombaji aliyechaguliwa na nakala ya fomu ya kuweka fedha benki itumwe kwa Mkuu wa Chuo, Chuo cha Misitu Olmotonyi, S. L. P. 943, ARUSHA, NUKUSHI: +255 27 250 9795 AU BARUA PEPE: fjshayo@yahoo.com Akaunti ya Benki ya Chuo ni JINA LA AKAUNTI: Principal Forestry Training Institute, NAMBA YA AKAUNTI: 40801200102, BENKI: NMB, TAWI: Clock Tower Arusha.

For English Version (Click Here!) - List_of_selected_students.pdf

Majina_ya_waliochaguliwa_Kujiunga_na_chuo_2014-15_

© 2018 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top