You Are Here: Home » Whats New » Mabalozi Wasifu Juhudi za Tanzania Katika Kukuza Utalii na Vita Dhidi ya Ujangili

Mabalozi Wasifu Juhudi za Tanzania Katika Kukuza Utalii na Vita Dhidi ya Ujangili

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Konchanke, ameipongeza Tanzania kwa juhudi zake katika suala zima la kupambana na ujangili wa Wanyamapori hususan mauaji ya Tembo.

Balozi Konchanke, alitoa pongezi hizo jana alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalli Mhe. Lazaro Nyalandu, ofisini kwake Wizara ya Maliasili na Utalii .

Balozi Konchanke, alifika ofisini kwa Waziri Nyalandu kwa mazungumzo ambapo walijadili juhudi za pamoja katika suala zima la kutokomeza ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo.
Waziri Nyalandu alimuarifu balozi Kunchanke juu ya juhudi ambazo Serikali ya Tanzania inafanya ili kukabilana na ujangili wa wanyampori husan mauaji ya tembo.

Balozi huyo wa Ujerumani hapa nchini aliahidi kushiriki katika Mkutano wa uhifadhi (Mkutano wa Tembo) utakaofanyika mjini Arusha tarehe 7 na 8 mwezi Novemba mwaka huu.

Balozi Konchanke alifuatana na mshauri wa masuala ya maendeleo wa ubalozi wa Ujerumani,  bibi Lena Thiede. Katika tukio jingine, Waziri Nyalandu pia alitembelewa na Waziri wa Italia hapa nchini Bwana Luigi Scotto. Balozi Scotto, aliipongeza Tanzania kwa namna inavyowapokea watalii kutoka nchini kwake kuja hapa nchini na kusifu juhudi za Tanzania katika suala zima la kukuza Utalii na kupambana na Ujangili wa Wanyamapori husan mauaji ya Tembo.

Balozi Scotto, na Waziri Nyalandu walizungumzia kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa makubaliano ya pamoja kuhusu kuwepo kwa ndege ya moja kwa moja kutoka Italia hadi Zanzibar kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii kutoka Italia kuja hapa nchini. Akizungumza kuhusu mchango wa Watalii hapa nchini, Waziro Nyalandu a amesemsa Watalii kutoka Italy ni asilimia sitini na mbili ya wageni wanaokuja nchini Tanzania.

Balozi huyo wa Ujerumani hapa nchini, Mheshimiwa Scotto, ameahidi kushiriki katika mkutano wa Tembo utakaofanyika mjini Arusha tarehe 7 na 8 mwezi November mwaka huu.

Akizungumzia zaidi kuhusu suala zima la Utalli, waziri Nyalangu alisema,. Wizara ya Maliasili na Utalii haina mpango wa kuongeza kodi ya tozo kwa watalii ili kutoa fursa ya kuendeleza Utalii hapa nchini.

Waziri Nyalandu alisisitiza kuwa, pamoja na janga la Ebola kuikumba Africa Magharibi na hivyo kuathiri Utalii barani Africa kiujumla, lakini ipo haja ya kuzidi kuitangaza Tanzani na kuifanya jumuia ya kimataifa kufahamu wazi ya kuwa Afrika ni bara nia si nchi, kuwa Tanzania hakuna Ebola hivyo watalii wawe huru kuitembelea nchi yetu katika sekita ya Utalii. 

© 2018 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top