You Are Here: Home » Whats New » KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI LITACHOCHEA UTALII

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI LITACHOCHEA UTALII

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania na Malawi zimetambua umuhimu wa kuimarisha biashara za mipakani ambao pia ni mkakati wa kukuza utalii

Ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika jijini Mbeya. Makamu wa Rais amesema kongamano hilo litawezesha kuzungumzia fursa na changamoto za kibiashara ikiwemo shughuli za utalii baina ya nchi hizo.

Makamu wa Rais amesema kuwa kongamano hilo litatoa fursa za vivutio vya utalii vilivyoko mipakani kutangazwa na kuimarishwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema kongamano hilo mbali ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Malawi pia ni kichochea cha kukuza utalii kwa mikoa ya mipakani.

Amesema Serikali kwa sasa inaboresha miundombinu ya maeneo ya vivutio vya utalii vya Nyanda za Juu kusini hivyo Kongamano hilo ni linafanyika muda muafaka kwa vile litawavutia   wafanyabiashara wa utalii kuja kuwekeza katika fukwe za ziwa Nyasa

Aidha, Naibu Waziri Mhe. Japhet Hasunga amesema Kongamano hilo linatoa fursa ya kutangazwa uzuri wa fukwe za ziwa Nyasa.

Naye, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Mhe.Henry Musa amesema leo imeandikwa historia kubwa kati ya nchi hizo mbili na anaamini kuwa kongamano hilo litasaidia nchi hizo kufunguka kiuchumi.

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top