You Are Here: Home » Whats New » IGP SIRRO ATAKA UMOJA VITA DHIDI YA UJANGILI

IGP SIRRO ATAKA UMOJA VITA DHIDI YA UJANGILI

Kamanda wa Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amezitaka Taasisi za Uhifadhi nchini kufanya kazi kwa umoja na vyombo vya usalama ili kuweza kutokomeza tatizo la ujangili nchini

Akizungumza jijini Dodoma wakati akifunga warsha ya mafunzo ya namna ya kupambana na vita dhidi ya Ujangili iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Shirika la PAMS Foundation na Wizara ya Maliasili na Utalii, IGP Sirro amesema vyombo vya usalama vina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Ujangili badala ya kudhani ni jukumu ya Wizara pekee.

“Hakuna mwenye jukumu zaidi ya mwingine kwenye kulinda maliasili zetu, hizi ni maliasili za Taifa lazima tuhakikishe hazipotei na wala hazitoroshwi

Awali Mkurugenzi Msaidizi wa uzuiaji ujangili na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi Taifa cha Kuzuia na Kupambana na Ujangili, Robert Mande ameeleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikishirikiana na Kikosi Kazi Taifa cha Kuzuia na Kupambana na Ujangili chini ya PAMS Foundation ambapo wamefanikiwa kukamata silaha 356,risasi 20,565, pamoja nav silaha za kivita kama vile short gun.

Aidha, meno ya tembo 211, vipande 413 wakiwemo   watuhumiwa 963 pia walikamatwa.


Aliongeza kuwa vita dhidi ya ujangili ni kubwa, hata hivyo kufuatia ushirikiano wa wananchi
pamoja vyombo vya usalam vimesaidia kupunguza tatizo la ujangili.

Katika warsha hiyo jumla ya washiriki 122 walikabidhiwa vyeti ikiwa ni ishara ya kufuzu mafunzo hayo yakihusisha Polisi, Watumishi kutoka TAWA, TFS, TAKUKURU pamoja DCI

© 2019 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top